Mtoto Wangu App
Suluhisho la malezi ya watoto wa kizazi hiki.Tunamsaidia mzazi kupata taarifa na msaada anaohitaji kuhusu mtoto wake
Kuhusu Sisi
Ifahamu Mtoto Wangu App
Ni mfumo maalumu unaomsaidia mzazi katika ufuatiliaji wa maendeleo ya mtoto katika maeneo mbalimbali kama ya kitabia, kijamii, kiakili, kielimu na maeneo mengine muhimu ya ukuaji wa mtoto;
Mfumo huu utatatua changamoto ya ufuatiliaji wa mtoto unaotokana na kutingwa kwa wazazi wengi kwenye shughuli mbalimbali za kimaisha kama vile za kiuchumi na kijamii.
Mzazi ataweza kujua maendele ya mtoto wake akiwa nyumbani au kazini au mahali popote na kupata takwimu iliyochakatwa kwa kina ikieleza hali ya maendeleo ya mtoto. Jiunge SasaMaendeleo ya Kiakili
Fuatilia maendeleo ya kiakili ya mtoto kwa urahisi kupitia vipengere mbalimbali vya kupima uwezo wa kiakili wa mtoto.
Maendeleo ya kitabia
Fuatilia maendeleo ya kitabia ya mtoto kwa urahisi kupitia vipengere mbalimbali vya kupima mwenendo wa tabia ya mtoto.
Maendeleo ya Kimwili
Fuatilia maendeleo ya kimwili ya mtoto kwa urahisi kupitia vipengere mbalimbali vya kuangazia namna mtoto anavyoujali mwili wake.
Maendeleo ya kijamii
Fuatilia maendeleo ya kijamii ya mtoto kwa urahisi kwa kuangalia namna anvyo shirikiana na jamii inayomzunguka na kujihusisha katika mambo ya kijamii.
Huduma Zetu
Huduma ya Mtoto Wangu ni kama zifuatazo
Huduma ya kwanza ya Mtoto Wangu Web-App
Kutambua maendeleo ya mtoto katika Nyanja zote
- Kiakili
- Kitabia
- Kimwili
- Kijamii
Huduma ya pili ya Mtoto Wangu Web-App
Kumsaidia mzazi kupata matokeo ya mtoto mtandaoni; Kumsaidia mzazi kupata matangazo yote muhimu kutoka shule ya mtoto wake na pia Kumsaidia mzazi kuuliza maswali yanayohusu malezi na makuzi ya mtoto na kupatiwa majibu.
Huduma ya tatu ya Mtoto Wangu Web-App
Kumsaidia mzazi kupata waalimu, walezi wa watoto, wanasaikolojia na kupata shule bora kutoka kila mkoa nchini
- Walimu wa masomo mbalimbali
- Washauri na wanasaikolojia mbalimbali
- Walezi mbalimbali wa watoto.
Huduma ya nne ya Mtoto Wangu Web-App
Kumsaidia mzazi kutambua kipawa cha mtoto wake
Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara (FAQs)
Haya ni maswali yaliyolizwa mara kwa mara na majibu yake
Mtoto wangu ni nini
Ni mfumo unaomsaidia mzazi katika malezi ya mtoto
Mnapatikana wapi
Tunapatikana Iringa nchini Tanzania lakini tunatoa huduma kote nchini.
Mtoto wangu inawahudumia watoto wa ngazi gani kielimu
Watoto wa kuanzia chekechea hadi kidato cha nne
Wasiliana Nasi
Je, untaka kujifunza zaidi au kupata ufafanuzi wa huduma zetu tafadhali wasiliana nasi kupitia taarifa hizi za mawasiliano au tutumie ujumbe moja kwa moja hapa!
Anuani yetu
S.L.P 000,
Mtaa wa Miyomboni,
Iringa (M), Tanzania.
Tupigie
+255763833671
Barua Pepe
info@mtotowangu.co.tz